The United Republic of Tanzania

SELF Microfinance Fund

Mshahara Loan

Jina La Mkopo

Mkopo wa Mshahara

Lengo la Mkopo

Kuwezesha Watumishi/Wafanyakazi kukidhi mahitaji binafsi ya nyumbani kama vile ununuzi wa vifaa vya nyumbani, mali, elimu ya juu nk.

Walengwa

Watumishi wa Umma wenye mshahara na uajiri wa kudumu au wa mkataba wanaofanya kazi kwenye Serikali Kuu, Manispaa, Halmashauri, au taasisi yoyote nyingine ya Serikali.

Maelezo/Vipengele vya Mkopo

Muda wa Mkopo: Mpaka miezi 84 yaani miaka 7.

Ratiba ya Mrejesho

Kila mwezi

Kiwango Cha Mkopo:

  1. Kuanzia TZS 100,000
  2. Mpaka TZS 70,000,000

Mahitaji ya Kuwasilisha Kufanya Tathmini wa Mkopo.

  1. Mkopaji atimize vigezo vya ustahili.
  2. Mkopaji atimize sharti la kiwango cha mshahara wa mwezi cha kubaki baada ya makato (Monthly salary take home rule).
  3. Fomu ya Maombi ya Mkopo iliojazwa kikamilifu.
  4. Fomu ya Dhamana ya Pamoja iliojazwa na kusainiwa kikamilifu.
  5. Hati/Slipu ya mshahara orijino ya karibuni (Latest original pay slip).
  6. Fomu ya Tamko la Mfanyakazi iliosainiwa sahihi.
  7. Nyaraka za Mjue Mteja Wako (KYC Documents).