The United Republic of Tanzania

SELF Microfinance Fund

Mkopo wa Kilimo

Lengo La Mkopo

Kutatua changamoto nyingi za kifedha za watu/kampuni/taasisi mbalimbali zinazohusika katika mnyororo mzima wa thamani wa Kilimo.

Walengwa

Benki za Biashara, Benki za Jamii, Benki za Fedha Ndogo (Microfinance Banks), Taasisi za Fedha Ndogo (Microfinance Institutions), SACCOS, na VICOBA zinazokopesha wakulima na wafanyabiashara kwenye myororo wa thamani wa Kilimo.

Maelezo/Vipengele vya Mkopo

Muda wa Mkopo: Mpaka miezi 12.

Kiwango Cha Mkopo: Kopa mpaka TZS Bilioni 2.

Mahitaji ya Kuwasilisha Kufanya Tathmini wa Mkopo

Benki

  1. Leseni hai ya Biashara ya Manispaa/Halmashauri.
  2. Leseni ya Benki kutoka Benki Kuu Ya Tanzania.
  3. Hati Safi ya TRA (Tax Clearance Certificate).
  4. Hati ya Usajili Kampuni kutoka BRELA.
  5. Hati/Memoranda na Makala ya Makubaliano - Memorandum and Articles of Association (MEMART)
  6. Mrejesho wa kila mwaka BRELA.
  7. Nakala za Cheti cha Usajili VAT na Utambulisho wa Mlipa Kodi (TIN).
  8. Azimio la Bodi Kukopa.
  9. Sera ya Mikopo
  10. Taarifa ya Ukaguzi wa Fedha isiopungua mwaka mmoja nyuma.
  11. Makadirio ya Mzunguko wa Fedha wa mwaka/miaka ijayo.
  12. Mpango wa Biashara (Business plan)

Makampuni ya Fedha Ndogo (Microfinance Companies)

  1. Leseni hai ya Biashara ya Manispaa/Halmashauri.
  2. Hati Safi ya TRA (Tax Clearance Certificate).
  3. Wasifu (CVs) za Bodi ya Wakurugenzi na Timu ya Usimamizi (Management Team).
  4. Hati ya Usajili Kampuni kutoka BRELA.
  5. Hati/Memoranda na Makala ya Makubaliano - Memorandum and Articles of Association (MEMART).
  6. Mrejesho wa kila mwaka wa BRELA.
  7. Hati za Wanahisa (Shareholders Share Certificate).
  8. Nakala za Cheti cha Usajili VAT na Utambulisho wa Mlipa Kodi (TIN).
  9. Azimio la Bodi Kukopa.
  10. Sera ya Mikopo.
  11. Taarifa ya Ukaguzi wa Fedha isiopungua mwaka mmoja nyuma.
  12. Makadirio ya Mzunguko wa Fedha wa mwaka/miaka ijayo.
  13. Mpango wa Biashara (Business Plan).

SACCOS

  1. Leseni hai ya Biashara ya Manispaa/Halmashauri.
  2. Hati Safi ya TRA (Tax Clearance Certificate).
  3. Wasifu (CVs) za Bodi ya Wakurugenzi na Timu ya Usimamizi (Management Team).
  4. Hati ya Usajili Kampuni kutoka BRELA.
  5. Cheti cha Dhima ya Juu (Certificate of Maximum Liability).
  6. Azimio la Bodi Kukopa.
  7. Sera ya Mikopo.
  8. Taarifa ya Ukaguzi wa Fedha isiopungua mwaka mmoja nyuma.
  9. Taarifa ya Ukaguzi wa Fedha ya COASCO isiopungua mwaka mmoja nyuma.
  10. Makadirio ya Mzunguko wa Fedha wa mwaka/miaka ijayo.
  11. Mpango wa Biashara (Business Plan).