The United Republic of Tanzania

SELF Microfinance Fund

Mkopo wa Mkulima

Jina la Mkopo

Mkopo wa Mkulima

Lengo la Mkopo

Kusaidia Wakulima Wadogo (small holder farmers), Biashara Ndogo ndogo na za Kati (MSME’s) kwa mahitaji ya mtaji wa kazi wa kila siku (Working Capital).

Walengwa

Wakulima na Wafugaji wadogo, Mawakala wa Zana za Kilimo, Wachukuaji bidhaa za Kilimo (Offtakers) wa mazao ya Chakula na ya Biashara, Mbogamboga, Maua na wa Mifugo ya Kuku, Ngombe wa Maziwa na wa Nyama, Nguruwe nk.

Maelezo/Vipengele vya Mkopo

Muda Wa Mkopo: Mpaka miezi 24.

Ratiba ya Mrejesho:

Kila mwezi au kwa Mkupuo kulingana na aina ya biashara (Balloon Payment)

Kiwango Cha Mkopo:Kopa kuanzia TZS Milioni 1 Mpaka TZS Bilioni 1.

Mahitaji ya Kuwasilisha Kufanya Tathmini wa Mkopo.

Kampuni ya umiliki Binafsi (Proprietorship Firm)

 1. Valid Business license
 2. Business Registration (where applicable)
 3. TIN Certificate
 4. Income Tax Clearance
 5. Proof of ownership
 6. Audited/management books of accounts (where applicable)

Kampuni ya Dhima Yenye Kikomo (Limited Liability Company).

 1. Leseni ya Biashara (Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara).
 2. Hati ya Usajili Kampuni (BRELA).
 3. Hati/Memoranda na Makala ya Makubaliano - Memorandum and Articles of Association (MEMART).
 4. Nakala ya Cheti cha Mlipa Kodi cha Kampuni (Company TIN Certificate).
 5. Hati Safi ya TRA (Tax Clearance Certificate).
 6. Azimio la Bodi/Wakurugenzi/Menejiment kukopa.
 7. Taarifa ya Ukaguzi wa Fedha (Pale Inapostahili) au Mahesabu ya Biashara isiopungua mwaka mmoja nyuma.

Kampuni ya Umiliki wa Ubia (Partnership Firm)

 1. Hati ya Ubia (Partnership Deed).
 2. Hati ya Usajili wa Kampuni (BRELA).
 3. Hati/Memoranda na Makala ya Makubaliano - Memorandum and Articles of Association (MEMART).
 4. Nakala ya Cheti cha Mlipa Kodi cha Kampuni (Company TIN Certificate).
 5. Azimio la Wabia kukopa.
 6. Hati Safi ya TRA (Tax Clearance Certificate).
 7. Taarifa ya Ukaguzi wa Fedha (Pale Inapostahili) au Mahesabu ya Biashara isiopungua mwaka mmoja nyuma.

Wakulima wasio na Leseni (Mfano Wafugaji)

 1. Taarifa ya Ukaguzi wa eneo (Physical Visit Report) yenye Picha za eneo la shughuli inapofanyika.
 2. Barua ya utambulisho ya Serikali ya Mtaa.
 3. Dhamana ya 125% ya mkopo.