The United Republic of Tanzania

SELF Microfinance Fund

Mkopo wa Imarika

Lengo la Mkopo

Kusaidia Biashara Ndogo na za Kati (SME’s) kwa mahitaji ya mtaji wa kazi wa kila siku (Working Capital).

Kusaidia Taasisi/Kampuni/Mfanyabiashara kupata vifaa (assets) mbalimbali wanazohitaji za kusaidia kuboresha na kukuza biashara zao.

Walengwa

Taasisi Ndogo na za Kati za Biashara (MSMES’s) kama vile Makampuni, Kampuni za Ushirikiano (Partnership firms) na za Umiliki wa mtu mmoja (Single Proprietorship firms).

Maelezo/Vipengele vya Mkopo

Muda wa Mkopo Mpaka miezi 24.

Ratiba ya Mrejesho: Kila mwezi.

Kiwango Cha Mkopo:
Kopa kuanzia TZS Milioni 30 Mpaka TZS Bilioni 1.

Mahitaji ya Kuwasilisha Kufanya Tathmini wa Mkopo

Kampuni ya Umiliki Binafsi (Single Proprietorship)

 1. Leseni hai ya Biashara ya Manispaa/Halmashauri.
 2. Usajili wa Biashara (Pale Inapostahili).
 3. Nakala ya Cheti cha Mlipa Kodi (TIN Certificate).
 4. Hati Safi ya TRA (Tax Clearance Certificate).
 5. Ushahidi wa Umiliki.
 6. Taarifa ya Ukaguzi wa Fedha (Pale Inapostahili) au Mahesabu ya Biashara isiopungua mwaka mmoja nyuma.

Kampuni ya Dhima Yenye Kikomo (Limited Liability Company)

 1. Leseni ya Biashara (Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara).
 2. Hati ya Usajili Kampuni (BRELA).
 3. Hati/Memoranda na Makala ya Makubaliano - Memorandum and Articles of Association (MEMART).
 4. Nakala ya Cheti cha Mlipa Kodi cha Kampuni (Company TIN Certificate).
 5. Hati Safi ya TRA (Tax Clearance Certificate).
 6. Azimio la Bodi/Wakurugenzi/Menejiment kukopa.
 7. Taarifa ya Ukaguzi wa Fedha (Pale Inapostahili) au Mahesabu ya Biashara isiopungua mwaka mmoja nyuma.

Kampuni ya Ubia

 1. Hati ya Ubia (Partnership Deed).
 2. Hati ya Usajili wa Kampuni kutoka BRELA.
 3. Hati/Memoranda na Makala ya Makubaliano - Memorandum and Articles of Association (MEMART).
 4. Nakala ya Cheti cha Mlipa Kodi cha Kampuni (Company TIN Certificate).
 5. Azimio la Wabia kukopa.
 6. Hati Safi ya TRA (Tax Clearance Certificate).
 7. Taarifa ya Ukaguzi wa Fedha (Pale Inapostahili) au Mahesabu ya Biashara isiopungua mwaka mmoja nyuma.