The United Republic of Tanzania

SELF Microfinance Fund

Mkopo wa Makazi

Jina la Mkopo

Mkopo wa Makazi

Lengo la Mkopo

Kutoa uwezeshaji wa makazi ya heshima kwa kaya zisizo na fungu kubwa (lump sum) kwa ajili ya ujenzi wa nyumba.

Kusaidia wamiliki wa nyumba kuboresha nyumba zao kwa kufanya ukarabati na matengenezo.

Kupitia Mkopo mdogo huu wa nyumba (Micro housing product), SELF MF inatekeleza Mpango wa Serikali kufanikisha nyumba bora za makazi kwa raia wote wa Tanzania [waliopo vijijini na mijini].

Walengwa

Wananchi wenye kipato cha chini na cha kati ambao zaidi wanaishi maeneo ya vijijini au wanakaa kwenye maeneo ambayo hayajapangwa katika miji mikubwa

Mkopo Mdogo wa Nyumba utakidhi mahitaji yafuatayo ya mkopaji;

  1. Kuboresha nyumba iliopo tayari imejengwa.
  2. Kukarabati/kurekebisha nyumba iliopo tayari.
  3. Kujenga nyumba mpya.
  4. Kununua kiwanja kiliochopimwa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba.
  5. Kununua nyumba ambayo ilishajengwa, kutoka kwa mjengaji au muuzaji mwingine yeyote.

Maelezo/Vipengele vya Mkopo

Muda Wa Mkopo: Kuanzia mwaka 1 Mpaka miaka 3.

Ratiba ya Mrejesho

Kila mwezi

Kiwango Cha Mkopo:

Kuanzia TZS 1,000,000 Mpaka TZS 30,000,000

Mahitaji ya Kuwasilisha Kufanya Tathmini wa Mkopo.

  1. Mkopaji atomize vigezo vya ustahili.
  2. Rejeleo Zuri (Favorable reference) kutoka kwa mtu/mfanyabiashara asie ndugu (mfano; wazabuni, wateja nk) na majirani nyumbani.
  3. Nakala za Kitambulisho, Cheti cha Mlipa Kodi (TIN), Leseni stahiki.
  4. Picha za Dhamana iliowekwa.
  5. Historia ya kukopa/mikopo iliopita.
  6. Tathmini ya kiwango cha madeni yaliopo. Mteja awe na uwezo wa kupata mdhamini anaekubalika.