The United Republic of Tanzania

SELF Microfinance Fund

Mkopo wa Kopa Ada

Jina La Mkopo

Mkopo wa Kopa Ada

Lengo la Mkopo

Kutoa msaada wa kifedha kwa wanafunzi ambao bila hilo wangeshindwa kuhudhuria shule kwa kukosa ada.

Kusaidia wazazi na walezi kulipa ada kwa wakati mara zote.

Kusaidia shule ziwe na ukwasi wa kutosha (sufficient liquidity) kuendesha shughuli zao bila usumbufu.

Walengwa

Wazazi/Walezi wenye watoto katika shule za msingi na za sekondari.

Maelezo/Vipengele vya Mkopo

Muda Wa Mkopo: Kuanzia muhula 1 Mpaka mihula 3

Ratiba ya Mrejesho

Kila mwezi

Kiwango Cha Mkopo:

Kuanzia TZS 100,000 Mpaka TZS 3,000,000 kutegemeana na mpangilio wa ada wa shule husika.

Mahitaji ya Kuwasilisha Kufanya Tathmini ya Mkopo

  1. Mkataba wa Makubaliano (MOU) na shule husika.
  2. HifadhiData (Database) ya wazazi/walezi wote kutoka shule.
  3. Fomu ya Maombi ya Mtandao iliojazwa kikamilifu.