Oktoba 28, 2026, Afisa Mtendaji Mkuu wa SELF Microfinance Fund (SELF MF),
Ms. Santiel Yona, amekutana na wahariri na waandishi wa habari kwa lengo la
kuongeza uelewa wa umma kuhusu huduma zinazotolewa na SELF MF na kuimarisha
ushirikiano na vyombo vya habari katika kusambaza taarifa sahihi kuhusu
huduma hizo kwa jamii.
Kikao hicho ni sehemu ya juhudi za SELF MF za kuimarisha mawasiliano na wadau
wa habari ili kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi kuhusu huduma za
kifedha zinazotolewa na taasisi hiyo.
