Matangazo
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI - AFISA MAUZO (SALES EXECUTIVE)
Mfuko wa SELF ni Taasisi ya Serikali iliyo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango inayotoa huduma za mikopo yenye masharti nafuu pamoja na bima. Mfuko unakaribisha maombi ya kazi kwa Watanzania wenye sifa na uwezo za kujaza nafasi 5 za Afisa mauzo wa Bima (Sales Executive) kwa kipindi /muda maalum (specified period) katika Mkoa wa Dar es salaam
SIFA ZA MWOMBAJI
- Cheti au stashahada au shahada ya bima, utawala wa biashara, masoko na mauzo
- Cheti cha kidato cha nne au sita.
- Awe na uwezo wa kuzungumza Kiswahili na Kiingereza kwa ufasaha
- Awe na uwezo wa kushawishi na kujenga mahusiano
- Uzoefu wa kuuza huduma za bima au huduma za kifedha nyinginezo utazingatiwa.
- Awe na ari ya kupata kipato kikubwa kwa kufanya mauzo mengi
Muombaji awasilishe barua ya maombi na wasifu unaojitosheleza (CV) wenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) wawili wa kuaminika mmoja awe ni Mfanyakazi wa Serikali
Maombi yatumwe kwa Barua Pepe, info@self.go.tz au katika Ofisi za Makao Makuu ya Mfuko wa SELF,Jengo la SELF MF, Barabara ya Obama, Nyumba na. 43. Tafadhahali wasilisha maombi yako kabla ya tarehe 13, Machi, 2023 saa 6 usiku